26.10.07 - ICTR/KAREMERA - MAHAKAMA YA ICTR IMEKATAA KUWASIKILIZA WATAALAM WA MASHTAKA

Arusha, 26 Octoba 2007 (FH) – Chemba ya mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji ya Rwanda ICTR inayoshughulika na kesi ya viongozi watatu wa chama tawala cha zamani imekata kuwasikiliza mashahid watatu wataalam wa mashtaka walioitwa na mashtaka ya kesi hiyo ambao walikwisha kutoa ushahidi wao katika kesi zingine katika mahakama ya kimataifa ya iliyokuwa Yugoslavia, ICTY, kama ilivyobainishwa na chanzo cha kisheria Ijumaa.

1 min 23Temps de lecture approximatif

 Ktika kesi hiyo inayoongozwa na rais wa mahakama jaji , Judge Dennis Byron, mwendesha mashtaka anategemea kumwita mmarekani Alison Des Forges, mwanahistoria na mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu, mwanasayansi wa masuala ya kijamii raia wa Ufaransa André Guichoua pamoja na mkenya Binaifer Nowrojee, mtaalam wa masuala ya unyanyasi wa kijinsia. Des Forges na Nowrojee ni watafiti katika shirika la kulinda haki za binadamu (HRW).

"Chemba hiyo ilitoa hitimisho la kwamba Alison Des Forges, André Guichoua na Binaifer Nowrojee hawataweza kukubalika kuitwa mashahidi wakitaalam", katika kesi hii, kama walivyosema majaji katika waraka wa maamuzi uliotolewa Alhamisi. Mbali na kujadili kuhusiana na uwezo pamoja na vigezo vya utaalam wa wasomi hao, chemba haijashawishika kuwakubali".

Chemba hiyo hiyo iliwahi kumkataa mtaalam wa kinyarwanda, mwanasheria Charles Ntampaka. aUamuzi huu utakuwa na matokeo yanayogusa moja kwa moja suala zima la muda kwa vile muda wa mashtaka wa kuwasilisha kesi yake utapungua. Mashtaka imekuwa ikiendesha kesi yake kwanzia Septemba 2005 na inatakiwa kumaliza mwishoni mwa mwaka huu. Na kama chemba itatoa muda unaolingana na ule iliyopewa mashtaka basi kesi hii haitoweza kukamilika kabla ya mwaka 2010.

Baraza la Umoja wa Mataifa lilishaomba mahakama ya ICTR kumaliza kesi zake za mahakama ya mwanzo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2008. Alhamisi wakati wa mkutano wa msemaji wa mahakama Roland Amoussouga na wandishi wa habari alitambua kuwa kesi hiyo haitoweza kumalizika katika muda ulioagizwa. Akipokea uwakilishi wa kidiplomasia hivi karibuni, rais wa mahakama jaji Byron aliongelea suala la kuwepo kwa kesi ambazo zitaendelea hadi miezi mitatu ya mwonzoni mwa mwaka 2009.

Kesi hii ambayo mwendelezo wake ulikuwa umefutwa inawahusisha rais wa chama cha MRND ambacho kilikuwa chama tawala mwaka 1994, Mathieu Ngirumpatse, rais msaidizi wa zamani, Edouard Karemera na katibu mkuu wa zamani wa chama hicho, Joseph Nzirorera. Wakishtakiwa kwa mauaji ya kimbari na makosa ya jinai, wote walikana kosa.

AS/
© Hirondelle News Agency